Home Azam FC AZAM FC YAWEKA REKODI TAMU KAGAME, KOCHA ATOA NENO

AZAM FC YAWEKA REKODI TAMU KAGAME, KOCHA ATOA NENO


VIVIER Bahati, Kocha Msaidizi wa Azam FC amesma kuwa vijana wake wanastahili pongezi kwa kuweza kutinga hatua ya nusu fainali na wanatakiwa waendelee kutambua kwamba kazi bado inaendelea.

Ni bao pekee la Idd Kipagwile staa wa Azam FC ambaye alipachika bao hilo dk 22 liliwafanya waweze kutinga jumla hatua ya nusu fainali mbele ya Messager FC ya Burundi.

SOMA PIABAADA YA KUTEMWA AZAM FC OBREY CHIRWA HUYOOO NAMUNGO FC

Katika kundi B la Kombe la Kagame 2021 linalofanyika Tanzania na kutumia viwanja viwili ambavyo ni ule wa Mkapa pamoja na Azam Complex, mabingwa watetezi ni KCCA ambayo ipo kundi moja na Azam ikiwa nafasi ya pili na pointi 3.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya kwanza katika kundi B imekusanya jumla ya pointi 4 huku Messager FC ikiwa imekusanya jumla ya pointi moja baada ya kucheza mechi mbili.

Bahati amesema:”Vijana wamepambana na wanastahili pongezi licha ya ushindi bado kazi inaendelea kwani tunahitaji kuweza kutwaa taji hili,”.

Inakuwa ni rekodi tamu ambayo imewekwa na Azam FC ambao wanaiwakilisha Tanzania, timu nyingine ni Yanga ambayo ipo kundi A ina pointi mbili pamoja na KMKM iliyo kundi B ina pointi moja.

SOMA NA HII  KINACHOMBEBA MTUPIAJI NAMBA MOJA BONGO HIKI HAPA