Home Simba SC BERNARD MORRISON ATAJA SIKU ANAYOIKUMBUKA NDANI YA SIMBA

BERNARD MORRISON ATAJA SIKU ANAYOIKUMBUKA NDANI YA SIMBA

 KIUNGO mshambuliaji wa Simba, Bernard Morrison amesema kuwa miongoni mwa vitu ambavyo anavikumbuka ndani ya Simba ni pamoja siku yake ya utambulisho iliyofanyika siku ya Simba day.

Nyota huyo aliibuka ndani ya Simba akiibukia Klabu ya Simba akitokea Klabu ya Yanga ambapo dili lake limekuwa na utata hasa suala lake la mkataba.


Mabosi wake wa zamani Yanga wanadai kwamba mchezaji huyo ni mali yao kwa kuwa alisaini dili la miaka miwili huku yeye akiweka wazi kwamba alisaini dili la miezi sita. 


Sakata lake ilitinga Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) ambapo lilisikilizwa kwa muda wa siku tatu kisha ikaamuliwa kwamba mchezaji huyo ni huru kwa kuwa kulikuwa na makosa ya kimkataba ikiwa ni pamoja na suala la saini na mhuri.


Morrison amesema:”Ninaikumbuka siku ile ya utambulisho kwa mashabiki Uwanja wa Mkapa, namna ambavyo walinipokea na kunishangilia ilikuwa furaha kwangu na ipo Kwenye kumbukumbu zangu, ” .

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI YA CAF...SIMBA WAISHTUKIA JAMBO HILI IVORY COST....