Home Uncategorized DECLAN RICE AGOMEA KUIBUKIA MANCHESTER UNITED

DECLAN RICE AGOMEA KUIBUKIA MANCHESTER UNITED

 


NYOTA wa Klabu ya West Ham United, Declan Rice imeelezwa kuwa amemwambia rafiki yake kwamba hana mpango wa kujiunga na Klabu ya Manchester United. 

Nyota huyo amekuwa akihusishwa kujiunga na Klabu ya Manchester United inayonolewa na Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer ambaye amekuwa akikubali uwezo wake.

Kwa mujibu wa The Mirror, raia huyo wa England amesema kuwa atafurahi zaidi ikiwa atakwenda Stamford Bridge kuliko kuwa mikononi mwa Ole Gunner Solskjaer. 

Chanzo hicho kimefafanua kuwa mchezaji huyo anapenda kufanya kazi na rafikiye Mason Mount ambaye yupo Chelsea. 

“Anahitaji kwenda Chelsea kuliko Manchester United kwa kuwa yupo Mason Mount ambaye ni rafiki yake, hivyo atafurahi akifanya naye kazi” ilieleza taarifa hiyo.

SOMA NA HII  WAWILI NAMUNGO KUIKOSA COASTAL UNION KESHO