Home Uncategorized WAWILI NAMUNGO KUIKOSA COASTAL UNION KESHO

WAWILI NAMUNGO KUIKOSA COASTAL UNION KESHO


 NAMUNGO FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Hemed Morroco kesho Desemba 31 itakuwa na kazi ya kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union.

Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Majaliwa,Namungo iliibuka na ushindi wa bao 1-0 lilipachikwa na kinara wa mabao ndani ya kikosi hicho, Bigirimana Blaise.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Namungo FC, Kidamba Namlia amesema kuwa wachezaji wapo tayari na kila kitu kinakwenda sawa wanasubiri wakati ufike.

“Tupo sawa na kila kitu kinakwenda sawa, kuna baadhi ya wachezaji ambao tutawakosa ndani ya kikosi ikiwa ni pamoja na beki Kristom na mshambuliaji Adam Salamba.

“Krmstom yeye ni mgonjwa na Salamba yeye bado hajarejea kwenye ubora wake hivyo wapo Dar wakiendelea na matibabu,” amesema.

SOMA NA HII  LIVERPOOL: WATFORD WALITUVURUGA KINOMA