Home Uncategorized ISHU YA MAJEMBE YANAYOTUA AZAM FC IMEKAA NAMNA HII

ISHU YA MAJEMBE YANAYOTUA AZAM FC IMEKAA NAMNA HII


 UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa utaongeza nyota wawili ndani ya kikosi hicho kwa ajili ya kuongeza nguvu ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho.


Tayari Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina imemalizana na mshambuliaji mmoja ambaye ni Mpiana Monzinzi raia wa Congo aliyekuwa anakipiga ndani ya FC Lupopo.


Nyota huyo amekuja kubeba mikoba ya Thiery Akono Akono ambaye ametimkia zake Malysia baada ya kupata dili huko.


Miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuwa kwenye rada za Azam FC ni pamoja na Perfec Chwikwende wa FC Platinum pamoja na kipa namba moja wa Biashara United, Daniel Mgore.


Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kuhusu Chikwende bado hawajafanya mazungumzo naye na kuhusu Mgore pia.

“Tutafanya usajili mzuri kwani sifa ya timu kubwa ni kusajili, wakati ukifika kila kitu kitakuwa wazi,” .

SOMA NA HII  KAKOLANYA AIBUKA NA KALI YA SIKU SIMBA