Home Simba SC LWANGA AONDOLEWA SIMBA

LWANGA AONDOLEWA SIMBA


JINA la kiungo mkabaji wa klabu ya Simba, Taddeo Lwanga limeondolewa katika orodha ya wachezaji waliosajiliwa na Simba ndani ya kipindi cha dirisha dogo na kukabidhiwa kwa Shirikisho la soka Tanzania TFF.kwa ajili ya kutumika katika mzunguko wa pili wa ligi.

Lwanga alitambulishwa rasmi na Simba Desemba 2, mwaka jana kama sehemu ya mbadala wa Mbrazili, Gerson Fraga na kukaa nje kwa muda mrefu kabla ya kupewa nafasi kwenye michezo ya kombe la Mapinduzi iliyofanyika mapema Januari mwaka huu.

Simba  imewasilisha majina mawili pekee kama sehemu ya wachezaji waliowasajili ndani ya kipindi cha usajili wa dirisha dogo, majina hayo ni; Tatenda Perfect Chikwende raia wa Zimbabwe na Mkongomani Doxa Gikanji.

Chikwende ametokea ndani ya kikosi cha FC Platinum huku Gikanji yeye akiwa ametokea ndani ya kikosi cha DC Motema Pembe.

SOMA NA HII  KUELEKEA MECHI NA VIPERS...MBRAZILI ABADILI 'GIA ANGANI' SIMBA....AINGIZA MBINU ZA KIMAFIA...