Home Yanga SC PACHA WA SAIDO YANGA AANZA SAFARI KUJA TANZANIA

PACHA WA SAIDO YANGA AANZA SAFARI KUJA TANZANIA


MSHAMBULIAJI mpya wa kimataifa wa Yanga raia wa Burundi, Fiston Abdoul Razak anayecheza kama pacha wa Said Ntibazonkiza ‘Saido’ kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Burundi, tayari ameanza safari ya kuja Tanzania kwa ajili ya kujiunga na kambi ya kikosi hicho inayojiandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Mshambuliaji huyo ni miongoni mwa nyota watatu waliokamilisha usajili wa kujiunga na kikosi cha Yanga katika dirisha dogo la usajili lililofungwa Januari 15.

Nyota huyo anatajwa kuwa hatari hasa anapocheza na pacha wake Saido ambapo akiwa na kikosi cha Burundi katika michezo ya kufuzu michuano ya AFCON amefanikiwa kuweka kambani mabao sita, hivyo kuongoza chati ya wafungaji pamoja na mshambuliaji wa timu ya taifa ya Nigeria na klabu ya Manchester United Odion Ighalo.

Akizungumzia kuhusu ujio wa nyota huyo kabla ya kusimamishwa majukumu yake, Ofisa habari wa klabu ya Yanga Hassani Bumbuli amethibitisha kuwa nyota huyo yupo njiani kuja kujiunga na wenzake na kuwaomba Wanayanga wajitokeze kwa wingi kama ilivyo kawaida yao

“Mshambuliaji wetu, Fiston Abdoul Razak anatarajiwa kuwasili nchini hivi karibuni akitokea kwao Burundi kwa ajili ya kujiunga na kambi ya Yanga inayoendelea kujiandaa na michezo ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara chini ya kocha Cedric Kaze.

“Kama kawaida yetu Wanayanga tunaomba mjitokeze kwa wingi kwa ajili ya mapokezi hayo,” alisema Bumbuli.

SOMA NA HII  CAS YAPANGA SIKU YA KUSIKILIZA KESI YA MORRISON, SAKATA KUANZA UPYA