Home Ligi Kuu PAWASA: BEACH SOCCER KUJA NA BONANZA, UDHAMINI TATIZO KUBWA

PAWASA: BEACH SOCCER KUJA NA BONANZA, UDHAMINI TATIZO KUBWA


 BONIFACE Pawasa, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania ya Beach Soccer amesema kuwa kwa sasa wana mpango wa kuandaa bonanza maalumu ambalo linatarajiwa kufanyika Januari 31.


Pawasa ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya michezo akiwa anachambua kwenye gazeti la michezo la Championi aliwahi kufanya vizuri ndani ya Klabu ya Simba, 2003 ambapo kikosi chao kiliweza kutinga hatua ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kikosi hicho cha msimu wa 2003, kipa alikuwa ni Juma Kaseja ambaye kwa sasa anakipiga ndani ya KMC akiwa ni nahodha.

Amecheza pia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars ambayo kesho itakuwa na kazi nchini Cameroon  kwenye mchezo wa Michuano ya Chan ambayo inashirikisha wachezaji wa ndani na itacheza dhidi ya Zambia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Pawasa amesema kuwa kuna mipango mingi katika kukuza na kuimarisha Beach Soccer jambo ambalo linafanyiwa kazi kwa ukaribu.

“Januari 31 tunatarajia kutakuwa na bonanza pale Escape One, ambalo litaitwa Dar Beach Soccer lengo ni kufikisha elimu kwa wananchi waelewe kanuni na sheria za Beach Soccer.

“Utakuwa ni wakati wa kila mmoja kujifunza sheria za Beach Soccer pamoja na kuzijua kanuni zake ambapo ni mchezo unaokua kwa sasa ndani ya Afrika, hivyo ni wakati wa kila mmoja kujifunza na kuutambua.

“Tatizo kubwa kwenye Beach Soccer ni kwamba hatuna udhamini hivyo wadau wajitokeze kwa wingi na kutupa sapoti ili kupeperusha bednera ya Tanzania,” .

SOMA NA HII  KMC HESABU ZAO KWA SASA NI DHIDI YA NAMUNGO