Home Yanga SC TAMBWE:FISTON ATAFANYA MAAJABU NDANI YA YANGA

TAMBWE:FISTON ATAFANYA MAAJABU NDANI YA YANGA

[the_ad id="25893"]

MSHAMBULIAJI wa zamani wa Klabu ya Yanga, Amiss Tambwe amesema kuwa usajili wa nyota mpya, Fiston Abdurazak utaiongezea makali safu ya ushambuliaji ambayo ilikuwa na tatizo la umaliziaji wa nafasi za kufunga.

Kwenye usajili wa dirisha dogo Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze imemalizana na Fiston raia wa Burundi kwa dili la miezi sita.

Tambwe ambaye amewahi kucheza kwenye timu zote zenye maskani ya pale Kariakoo Simba na Yanga amesema kuwa ikiwa ataweza kutibu yale makosa ya timu hiyo basi atafanya makubwa ndani ya kikosi hicho kinachowania ubingwa wa ligi.

“Kusajiliwa kwa Fiston ndani ya Yanga kunakwenda kuzalisha mabao mengi ndani ya kikosi hicho kwa kuwa walikuwa wanakosa mtu wa kutengeneza na kumalizia mipango.

“Kwa namna ambavyo ninamfahamu ninajua kwamba atafanya mengi makubwa ambayo yatawapa mafanikio mabosi wa Yanga pamoja na mashabiki.

“Ni suala la kusubiri namna ambavyo atakwenda kufanya kazi na kuweza kujibu kwenye mfumo mpya wa timu yake ambayo anakwenda ila kwa upande wa kucheka na nyavu hilo analijua na anaweza kuwa msaada ndani ya kikosi hicho,” amesema.

Fiston ameibukia ndani ya Klabu ya Yanga akitoka kucheza ndani ya Klabu ya ENPPI ya Misri.


Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na imefunga mabao 29.

SOMA NA HII  YANGA: HATUNA HOFU DHIDI YA SIMBA

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here