Home Uncategorized YANGA: HATUIOGOPI SIMBA SISI

YANGA: HATUIOGOPI SIMBA SISI


NAHODHA Msaidizi wa Yanga, Juma Abdul amesema kuwa kutolewa kwao kwenye hatua ya nusu fainali na Mtibwa Sugar ni matokeo ya uwanjani na wala hawajaikimbia Simba.
Abdul amerejea kwenye ubora wake kwa sasa na amekuwa mhimili kwenye safu ya ulinzi ana asisti moja kwenye ligi mpaka sasa akiwa amecheza jumla ya mechi tisa za ligi sawa na dakika 810.
Abdul amesema kuwa wachezaji walijituma mwanzo mwisho ila bahati ikawa mbaya kwao wakashindwa kulinda bao walilofunga mapema.
“Wachezaji walicheza kwa kujituma na walitimiza malengo yao ila bahati haikuwa kwetu kwani kusawazisha bao dakika za lala salama haikuwa na maana kwamba tunaiogopa Simba.
“Kwa sasa tumerejea Bongo tunajipanga kwa ajili ya mechi zetu za ligi pamoja na kombe la Shirikisho, kikubwa mashabiki watupe sapoti,” amesema Abdul.
SOMA NA HII  KLOPP ACHEKELEA KUITUNGUA ARSENAL MABAO 3-1