Home Uncategorized YACOUBA SONGNE HATIHATI KUIKOSA SIMBA LEO MAPINDUZI

YACOUBA SONGNE HATIHATI KUIKOSA SIMBA LEO MAPINDUZI


 CEDRICK Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake wote wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa fainali dhidi ya Simba huku akisubiri ripoti ya madaktari kuhusu kumtumia nyota wake Yacouba Songne.

Songne aliumia kwenye mchezo wa hatua ya nusu fainali ya kwanza dhidi ya Azam FC wakati Yanga ikilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 ndani ya dakika 90 na ilishinda kwa penalti 5-4 zilizoifanya iweze kutinga hatua ya fainali ambayo itachezwa leo Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Kaze amesema:”Kuhusu wachezaji wangu wote waliopo wapo vizuri na wanaendelea salama, ila ninadhani kwamba mchezaji wetu Yacouba nitasubiri ripoti ya madakatari kwa kuwa alipata majeraha kwenye mchezo wetu uliopita.

“Ninaamini kwamba tutakuwa na dakika 90 nzuri hivyo mashabiki wasiwe na mashaka sisi tupo vizuri na mwisho matokeo yatapatikana,” .

SOMA NA HII  LACAZETTE PASUA KICHWA, ARSENAL WAKUBALI KUKAA NAYE MEZA MOJA