Home Azam FC KIUNGO DOMAYO NJE YA UWANJA MWEZI MZIMA

KIUNGO DOMAYO NJE YA UWANJA MWEZI MZIMA


 KIUNGO wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina, Frank Domayo, anatarajiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na majeraha ya mguu.


 Domayo aliumia mguu kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe uliochezwa hivi karibuni na kumalizika kwa sare ya 1-1.


Hakuwa sehemu ya kikosi kilichocheza jana mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba wakati ikigawana pointi mojamoja kwa kufungana mabao 2-2, Uwanja wa Mkapa.


 Ofisa Habari wa Azam FC, Thabiti Zakaria, amesema: “Domayo atakaa nje kwa muda wa mwezi mmoja kwa majeraha ya mguu aliyoyapata kwenye mchezo wetu na TP Mazembe.

 

 “Huyu ni kati ya wachezaji mahiri kwenye kikosi cha Azam kutokana na jinsi ambavyo amekuwa akiitumikia timu hiyo uwanjani,” .




SOMA NA HII  BAADA YA KUONA MZIKI WA SIMBA 'UNAVYOKINUKISHA' MISRI....KOCHA AZAM 'KALAMBA MDOMO' KISHA AKAFUNGUKA HAYA MAPYA...