Home Azam FC NYOTA WANNE WA AZAM FC KUWAKOSA COASTAL UNION LEO

NYOTA WANNE WA AZAM FC KUWAKOSA COASTAL UNION LEO

 GEORGE Lwandamina,  Kocha Mkuu wa Azam FC leo atakiongoza kikosi chake kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union ya Tanga, Uwanja wa Mkwakwani. 

Wachezaji wake wanne atakosa huduma zao leo Februari 11 kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza zama zam Aristica Cioaba, Azam FC ilishinda mabao 2-0 Uwanja wa Azam Complex hivyo leo utakuwa mchezo wa kisasi kwa Coastal Union huku Azam FC wakilinda heshima. 

Nyota hao wanne ni pamoja na:-

Obrey Chirwa mshambuliaji huyu aliumia goti kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba,  Februari 7.

Emmanuel Charles nyota huyu nimgonjwa anasumbuliwa na malaria.

Hamahama nyota huyu anasumbuliwa na majeraha ya nyama ya paja.

Pamoja na kiungo Frank Domayo ambaye pia anasumbuliwa na goti na atakaa nje mwezi mzima akitibu jeraha hilo.

SOMA NA HII  BAADA YA KUMSHUSHA STRAIKA MCOLOMBIA....AZAM FC 'WALETA BALAA' LINGINE BONGO...