news

ADAM ADAM AFIKIRIA KUCHEZA NJE YA BONGO

admin February 26, 2021 12:47 pm


 NYOTA wa timu ya JKT Tanzania, Adam Adam ambaye kwa sasa yupo zake nchini Uturuki amesema kuwa mawazo yake ni kucheza nje ya nchi jambo ambalo analiomba liweze kutimia.

Adam ametupia mabao 7 ndani ya Ligi Kuu Bara ni kinara wa utupiaji ndani ya JKT Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed.

Yupo huko kwa ajili ya majaribio ya muda wa wiki moja ili aweze kupata nafasi ya kupata dili la moja kwa moja huko.

 Adam amesema kuwa anaamini kwamba mambo yatakuwa sawa kwake katika kutimiza ndoto yake ya kucheza soka la kulipwa nje ya Bongo.

“Ninafikiria kuhusu kucheza nje kwa sasa na sio ndani ya Bongo kwa kuwa nahitaji kupata changamoto mpya.

“Maombi yangu ni kuona kwamba hili nalo linafanikiwa kwa kwa ni ndoto yangu ya muda mrefu na nina amini itakuwa sawa,” amesema.

KASEKE:TUTAIFUNGA KEN GOLD KESHO MFARANSA WA SIMBA LEO KUFANYA MABADILIKO MAKUBWA KIKOSI CHA KWANZA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply