Home Azam FC AZAM FC WAFUNGUKIA ISHU YA KUMVUTA KWENYE BENCHI LA UFUNDI KOCHA MRUNDI

AZAM FC WAFUNGUKIA ISHU YA KUMVUTA KWENYE BENCHI LA UFUNDI KOCHA MRUNDI


 UONGOZI  wa Azam FC umeweka wazi kuwa kwa sasa hauna mpango wa kumrejesha kwenye benchi la ufundi, Etiene Ndayiragije raia wa Burundi baada ya kufutwa kazi ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars.

Ndayiragije alipewa kibarua cha kuinoa Stars akitokea Klabu ya Azam FC na aliteuliwa rasmi kuanza kuinoa timu hiyo Julai 2019.

Kwa sasa nafasi yake ndani ya Stars ipo chini ya Kocha Mkuu, Kim Poulsen raia wa Denrmark ambaye aliwahi kuwa kocha wa Stars 2012 hadi 2014 na 2011 hadi 2012 alikuwa kwenye soka la vijana.

Habari zilikuwa zinaeleza kuwa huenda Ndayiragije akarejeshwa ndani ya Azam FC kuongeza nguvu mbele ya Kocha Mkuu, George Lwandamina ambaye amebeba mikoba ya Aristica Cioaba aliyechimbishwa.

Abdulakarim Amin, Mtendaji Mkuu wa Azam FC amesema kuwa kwa sasa hawana mpango wa kumrejesha kocha huyo kwenye benchi la ufundi.

“Kwa sasa hakuna mpango wa kumrejesha Ndayiragije kwenye benchi letu la ufundi ambalo lipo chini ya Kocha Mkuu, George Lwandamina,”.

SOMA NA HII  AZAM FC YAZITAKA POINTI TATU ZA SIMBA KWA MKAPA