Home Azam FC AZAM FC:SIMBA HAWAJAWAHI KUTUFUNGA

AZAM FC:SIMBA HAWAJAWAHI KUTUFUNGA


 UONGOZI wa Klabu ya Azam FC umesema kuwa haujawahi kufungwa kihalali na wapinzani wao Simba ndani ya dakika 90 kwenye mechi walizokutana nao uwanjani.


Februari 7, Azam FC walilazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 dhidi ya Simba na kugawana pointi mojamoja Uwanja wa Mkapa.

Zakaria Thabit, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa kwenye mechi hizo tano ambazo walifungwa na Simba ni mechi moja walifungwa kihalali.

 “Katika mechi tano walizotufunga, naweza kusema ni moja tu walitufunga kihalali na ni ile ya FA ambayo kiujumla hatukuwa vizuri, nyingine ile ya mapinduzi tunajua penalti hazina mwenyewe.


“Ila Mechi tatu zote zilizosalia walibebwa na waamuzi, Kuna bao walitufunga mpira ulikuwa umetoka nje, ile nyingine Idd Chilunda alisawazisha mwamuzi akakataa, nyingine walifunga bao la offside wao wakakubali,” .


Simba imefikisha jumla ya pointi 39 kibindoni baada ya kucheza jumla ya mechi 17 huku Azam FC ikiwa na pointi 33 ipo nafasi ya tatu kwenye msimamo.
SOMA NA HII  AZAM FC MIKONONI MWA WASOMALIA KOMBE LA SHIRIKISHO