Home kimataifa BARCELONA WANYOOSHWA NA PSG

BARCELONA WANYOOSHWA NA PSG

 


LICHA ya kutupia bao la Kwanza mapema dakika ya 27 kwa mkwaju wa penalti,kupitia kwa Lionel Messi bado alikubali kichapo cha mabao 4-1 mbele ya PSG, mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya,  hatua ya 16.


Kylian Mbappe alitupia hat trick dakika ya 32,65 na 85 na msumari mmoja kwa PSG ulipachikwa na Moise Kean.


Wakiwa uwanja wao wa nyumbani, Camp Nou walipiga jumla ya mashuti 12 na manne yalilenga lango huku PSG wakipiga jumla ya mashuti 16 na 9 yalilenga lango.

SOMA NA HII  PAMOJA NA KUWA NAHODHA...MAGUIRE MAMBO YAWA MAGUMU MAN UTD...KOCHA WAKE ATOA KAULI NZITO ....