Home Ligi Kuu JKT TANZANIA BADO WAMO, HAWAJAKATA TAMAA

JKT TANZANIA BADO WAMO, HAWAJAKATA TAMAA

 KOCHA wa Klabu ya JKT Tanzania, Abdalah Mohamed,’Bares’  amesema kuwa bado hawajaka tamaa licha ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji, mchezo uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.


Matokeo hayo yanawafanya JKT Tanzania kufungwa na Dodoma Jiji, nje ndani msimu wa 2020/21 ambapo mchezo wa kwanza walifungwa mabao 2-0 na mchezo wa pili walipoteza kwa kufungwa mabao 2-1.

Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara ipo nafasi ya 14 ikiwa imekusanya pointi 20 baada ya kucheza mechi 19 huku Dodoma Jiji ikiwa nafasi ya 7 na pointi 28.

Dodoma Jiji imekuwa kwenye mwendo mzuri mzunguko wa pili kwa kushinda mechi mbili mfululizo, jana iliwanyoosha mabao 2-1 Coastal Union.

 Bares amesema kuwa bado wana nafasi ya kufanya vizuri kwenye mechi za mzunguko wa pili jambo ambalo linawapa nafasi za kupata ushindi ndani ya uwanja.

“Bado hatujaka tamaa kwenye mechi zetu kwa kuwa mzunguko wa kwanza kuna mapungufu ambayo tulikuwa nayo na tumeyafanyia kazi hivyo kwa mzunguko wa pili tuna amini tutafanya vizuri zaidi, mashabiki watupe sapoti,” alisema.

 Leo itakuwa Uwanja wa Jamhuri,Dodoma kusaka pointi tatu mbele ya Polisi Tanzania.

SOMA NA HII  MTIBWA SUGAR YAPANIA KUTEMBEZA DOZI