Home Simba SC SIMBA YAANZA SAFARI KUWAFUATA BIASHARA UNITED

SIMBA YAANZA SAFARI KUWAFUATA BIASHARA UNITED

 


KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes, leo Februari 16 kimeanza safari kuwafuata wapinzani wao Biashara United ya Mara.

 
Msafara wa mabingwa hao watetezi leo utatua Mwanza kisha kesho Februari 17 kitaibukia Mara kwa ajili ya maandalizi ya mwisho kwenye mchezo huo wa mzunguko wa pili.

Walipokutana kwenye mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Simba zama zile za Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga anuari 7, iliibuka na ushindi wa mabao 4-0.

Mchezo wao wa Ligi Kuu Bara unatarajiwa kuchezwa Februari 18, Uwanja wa Karume, Mara.

Biashara United ambao ni wenyeji wamecheza mechi 19 wao wamekuwa kwenye mwendo mzuri ambapo wapo nafasi ya 4 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 32 huku Simba ikiwa nafasi ya pili na pointi 39 imecheza mechi 19.

Baraza amesema kuwa ni mchezo mgumu ila watapambana kupata matokeo mbele ya Simba huku Gomes akiweka wazi kwamba wapo tayari na wanahitaji pointi tatu.


SOMA NA HII  ISHU YA KOCHA WA SIMBA KUONDOKA KAMBINI IKO HIVI.... ROBERTINHO AFUNGUKA KILA KITU