Home Simba SC WAPINZANI WA SIMBA WANABALAA

WAPINZANI WA SIMBA WANABALAA

 


NGOMA kundi A kwa sasa moto unazidi kuweka baada ya Al Ahly kushusha kichapo cha mabao 3-0 dhidi ya Al Merrik.


Mabao ya Al Ahly yalipachikwa na Mohamed Magdy dakika ya 57, Kahraba dakika ya 63 na Walter Bwalya dakika ya 71.


Ilikuwa ni Uwanja wa Taifa wa Cairo na ngoma inayofuata kwa Al Ahly inayoongoza Ligi kwa idadi ya mabao mengi ambayo ni matatu ikifuatiwa na Simba  ni dhidi ya Simba Februari 23 kwa Mkapa.

Al Ahly walipiga jumla ya mashuti 22 langoni kwa wapinzani wao Al Merrikh na katika hayo ni mashuti 6 yalilenga lango huku wapinzani wao walipiga jumla ya mashuti 8 na katika hayo manne yalilenga lango.

Umiliki wa mpira Al Ahly ilikuwa ni asilimia 71 na wapinzani wao asilimia 29 na walipiga jumla ya pasi 648 huku Al merrikh walipiga jumla ya pasi 272 hivyo Simba wana kazi ya kufanya ndani ya kundi A.

SOMA NA HII  ALIYESHINDWA NA MANGUNGU AFUNGUKA SIMBA...AFICHUA YALIYOTOKEA KWENYE KARATASI ZA MATOKEO...