Home Yanga SC YANGA YATAKA KUJITOA KWENYE KUSHIRIKI LIGI KUU BARA

YANGA YATAKA KUJITOA KWENYE KUSHIRIKI LIGI KUU BARA

 


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa ikiwa waamuzi wa mchezo wao wa kesho wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mtibwa Sugar watashindwa kuchezesha kwa haki na kuwanyima penalti ndani ya dakika 90 wataomba kujiondoa kwenye ligi.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela amesema kuwa wamekuwa wakionewa mara nyingi ndani ya uwanja na wanakaa kimya jambo ambalo linawaumiza.

Makamu huyo amesema:”Tulikuwa na mchezo dhidi ya Mbeya City kwenye sare ya kufungana bao 1-1, tulinyimwa penalti ya wazi ila mwamuzi aliwapa Mbeya City penalti pia, licha ya kuongea hilo hakuna hatua iliyochukuliwa na tumebaki tukionewa.

“Pia mchezo wetu dhidi ya Kagera Sugar kwenye sare ya kufungana mabao 3-3, tulinyimwa penalti ya wazi ambayo imetufanya tushindwe kufanya vizuri ndani ya uwanja.

“Mashabiki wetu wamekuwa wakikanywa na kusababisha tupigwe faini kwa wakati bila kusubiri ikiwa ni laki tano, laki tatu sasa hili  hatukubali ikiwa haki haitatendeka kwenye mchezo wetu wa kesho, tunaweza kuomba kujitoa kwenye ligi.

“Kikubwa tunahitaji haki ndani ya uwanja, kwani mashabiki wetu wanapenda kuona timu ikifanya vizuri ila pale ambapo wanashindwa kuona seheria 17 zinafuatwa basi wanakuwa na maamuzi ambayo yanasababisha tupigwe faini,” . 

SOMA NA HII  MORRISON NJIA NYEUPEEE YANGA....NABI AMPITISHA FASTA...ADAI TABIA ZAKE ZA KINIDHAMU SIO ISHU SANA KWAKE...