Home Ligi Kuu SIMBA vs PRISONS UWANJA WA MKAPA NI VITA YA KISASI

SIMBA vs PRISONS UWANJA WA MKAPA NI VITA YA KISASI


 MACHI 10, Uwanja wa Mkapa kutakuwa na vita ya kusaka pointi tatu, kati ya Simba dhidi ya Prisons.

Mchezo huo unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa ndani ya uwanja baada ya ule wa kwanza, Simba wakiwa ugenini kuonja joto ya jiwe kwa kufungwa zama zile za Sven Vandenbroeck.

Ikiwa Uwanja wa Nelson Mandela baada ya dakika 90 kukamilika ubao ulisoma Tanzania Prisons 1-0 Simba na ulikuwa ni mchezo wa kwanza kwa Simba kupoteza msimu wa 2020/21.

Itawakaribisha Uwanja wa Mkapa, Machi 10 huku timu zote mbili zikiwa na uhitaji wa kupata pointi tatu muhimu.

Kwenye msimamo, Simba po nafasi ya pili na pointi zake ni 45 baada ya kucheza jumla ya mechi 19 inawakaribisha Prisons ambao wapo nafasi ya 10 na pointi 27 baada ya kucheza jumla ya mechi 21.


Salum Kimenya, kiraka wa Tanzania Prisons amesema kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu ili kuweza kufikia malengo ambayo wamejiwekea.

“Muhimu kwenye mechi zetu zote ambazo tutaingia ndani ya uwanja ni kusaka pointi tatu kwa kuwa kila mmoja anahitaji kufikia malengo ambayo yapo.

“Kikubwa ni kwamba kila timu ni imara na inahitaji ushindi hiyo ipo hata kwetu pia mashabiki watupe sapoti kila kitu kitakuwa sawa,” .

Kwa upande wa Simba, nyota wao Shomari Kapombe amesema kuwa watazidi kupambana ili kufikia malengo na wanaamini kwamba mzunguko wa pili una ushindani mkubwa.

SOMA NA HII  AHMED ALLY - TUNAENDA TUKIWA NA AKILI TIMAMU NA UCHUNGU MZITO....HATUWEZI KUKUBALI KAMWE...