Home Ligi Kuu TATU BORA ZA MAGUFULI MSIMU WA 2015/16 ILIKUSANYA MABAO 162

TATU BORA ZA MAGUFULI MSIMU WA 2015/16 ILIKUSANYA MABAO 162


BAADA ya mpambanaji wa muda wote, John Pombe Magufuli aliyekuwa Rais wa awamu ya tano kuanza kazi Novemba 2015, Ikulu ya Magogoni Dar, ndani ya Ligi Kuu Bara aliweza kushuhudia ushindani mkubwa na timu tatu zilikuwa ndani ta tatu bora.

Leo hatunaye tena Magufuli baada ya Makamu wa  Rais, Samiah Suluhu ambaye kwa sasa ni Rais kutangaza taarifa hizo Machi 7.

Mwili wa Magufuli, unatarajiwa kupumzishwa Chato, Geita Machi 25 na leo upo Visiwani Zanzibar.

Hizi hapa ni tatu bora baada ya kumaliza ligi na ubingwa ulikuwa mikononi mwa Yanga ambayo kwa sasa inaongoza Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 50.

Baada ya timu zote kucheza jumla ya mechi 30 mambo yalikuwa namna hii:-Yanga ilikuwa nafasi ya kwanza na pointi zake 73 ilishinda jumla ya mechi 22, sare 7 na ilipoteza mechi moja, safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 70 na ile ya ulinzi iliruhusu mabao 20.

Nafasi ya pili ilikuwa ni Azam FC ilikusanya pointi 64 ilishinda mechi 18, sare 8 na ilipoteza 2. Mabao ilifunga 47 na ilifungwa 24.

Simba nafasi ya tatu ilikusanya pointi 62, ilishinda mechi 19, sare 5 na ilipoteza mechi 6. Safu ya ushambuliaji ilifunga mabao 45 na ile ya ulinzi iliruhusu mabao 17.

Alishuhudia tatu bora zikukusanya jumla ya mabao 162 ya kufunga na mabao 61 ya kufungwa.


SOMA NA HII  MSIMAMO WA LIGI KUU TANZANIA BARA