Home Ligi Kuu ASUKILE: SIMBA WALITUNYIMA MABAO MENGI DHIDI YA JKT

ASUKILE: SIMBA WALITUNYIMA MABAO MENGI DHIDI YA JKT

 


NAHODHA wa kikosi cha Tanzania Prisons, Benjamin Asukile amefunguka kuwa uchovu wa kusafiri umbali mrefu baada ya kucheza na Simba, ndiyo sababu kubwa iliyowafanya washindwe kupata ushindi mkubwa zaidi kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania.

Jumapili Prisons iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya kikosi cha JKT Tanzania, mchezo uliopigwa katika Uwanja wa Nelson Mandela Sumbawanga mkoani Rukwa.

Kabla ya mchezo huo Prisons walikuwa na kibarua kizito dhidi ya Simba kwenye mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam Machi 10.

Akizungumzia mchezo huo, Asukile amesema: “Tunashukuru Mungu kwa ushindi tulioupata katika mchezo wetu uliopita dhidi ya JKT Tanzania, ulikuwa mchezo mgumu na nikiri wapinzani wetu walikuwa bora hasa kwenye kipindi cha kwanza.

“Hii yote ilitokana na uchovu ambao tulikuwa nao baada ya kusafiri umbali mrefu baada ya mchezo wa sare dhidi ya Simba, lakini tulijitahidi kupambana na kipindi cha pili tukarejea kwenye kasi yetu ya kawaida, na naamini kama isingekuwa uchovu kikosi kingepata matokeo mazuri zaidi kwenye mchezo wetu” .

SOMA NA HII  BIASHARA UNITED WAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA NAMUNGO