Home Uncategorized HATMA YA SANCHEZ NDANI YA MANCHESTER UNITED HII HAPA

HATMA YA SANCHEZ NDANI YA MANCHESTER UNITED HII HAPA


OLE Gunnar Solskjaer, Meneja wa Manchester United amesema kuwa anataka mshambuliaji wake machachari, Alexis Sanchez abaki ndani ya kikosi hicho.

Solskjaer kesho atakuwa kibaruani kumenyana na Wolves ukiwa ni mchezo wake wa pili baada ya kufungua pazia na Chelsea pale Old Trafford na alishinda kwa mabao 4-0.

Sanchez amekuwa akihusishwa kuwaniwa na timu za Italia na inaonekana hana nafasi ya kucheza ndani ya kikosi cha kwanza United.

Dirisha la Ulaya litakavyofungwa Septemba 2 huenda likamhusu licha ya mshahara kuwa kikwazo.


 “Alexis ni mchezaji mzuri, ana weledi amerejea kufanya kazi na sisi ni sehemu ya kikosi chetu na tuna mpango naye,hatuna washambuliaji wengi, hvyo atatufaa ndani ya kikosi,” amesema.

SOMA NA HII  MOLINGA AACHWA BONGO,HIKI HAPA AMESEMA