Home Simba SC BAADA YA KIMYA KIREFU..SALUM MBONDE AIBUKA NA HAYA KUHUSU SIMBA SC

BAADA YA KIMYA KIREFU..SALUM MBONDE AIBUKA NA HAYA KUHUSU SIMBA SC

 


BEKI wa zamani wa Simba, Salum Mbonde amesema timu hiyo itafanya makubwa mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi kwamba endapo wachezaji watajitoa zaidi na kuongeza umakini kila wanapocheza.

Amesema kwamba Simba imeonyesha nia ya kufanya mapinduzi kwenye mechi za CAF jambo ambalo ameliambia kwamba linawezekana na mastaa wa timu hiyo waongeze nguvu na umakini wa kutamani mafanikio zaidi.

Amesema japokuwa anatambua michuano hiyo kuwa migumu na yenye ushindani, lakini mwanzo wa Simba umempa matumaini ya kuona hakuna jambo linaloshindikana penye nia ya kuhitaji kitu.

“Simba ipo vizuri, imejiandaa kikamilifu kwa kile kinachoonekana uwanjani, lakini mastaa wasiishie hapo wanatakiwa kuongeza umakini kila mechi, kwani kila wanaposhinda ushindani unakuwa mkubwa na wapinzani wao wanakuwa wanawatazama kwa jicho makini,” amesema na ameongeza kuwa;

“Kiukweli naona Simba itafika mbali kwenye michuano ya CAF, kwanza hatua waliofikia inawajengea ujasiri wachezaji kwamba inawezekana, lakini pia timu pinzani kuwaheshimu kwamba sio timu ya kubezwa, hapo mpira utachezwa wa maana,”amesema.

Mbonde tangu aachane na Simba kutokana na kusumbuliwa na majeraha, hakurudi tena kucheza na sasa anasomea Jordan University kilichopo mkoani Morogoro, ambako anasomea mambo ya utawala.

SOMA NA HII  SKAUTI SIMBA:- KLABU HAINA PESA YA KUSAJILI WACHEZAJI WA MAANA...