Home Ligi Kuu KOCHA BIASHARA UNITED KUIBUKIA KAGERA SUGAR

KOCHA BIASHARA UNITED KUIBUKIA KAGERA SUGAR


FRANCIS Baraza, Kocha Mkuu wa Biashara United anatajwa kumalizana na mabosi wa Kagera Sugar ambayo imemfuta kocha wao Mecky Maxime.

Maxime amefutwa kazi ndani ya kikosi hicho kwa kile ambacho kimeelezwa kuwa na mwendo mbovu wa timu hiyo ndani ya uwanja kwa msimu wa 2020/21.

Mchezo wake wa mwisho kukaa kwenye benchi kabla ya kufutwa kazi ilikuwa Uwanja wa Kaitaba ambapo timu yake iliyeyusha pointi tatu kwa kufungwa na Namungo FC.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-1 Yanga jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Kagera Sugar kuamua kuachana naye jumlajumla.

Habari zimeeleza kuwa Baraza ambaye mchezo wake wa ligi uliopita ndani ya Biashara United alikusanya pointi tatu mbele ya Ihefu FC.

Baraza mwenyewe amesema kuwa ikiwa utaratibu utakamilika basi jambo lolote linaweza kutokea.

SOMA NA HII  TANZANIA KUPELEKA TIMU NNE CAF, TFF YAFAFANUA TIMU ZITAKAZOKWENDA