Home Simba SC LUIS: KAZI BADO INAENDELEA KIMATAIFA

LUIS: KAZI BADO INAENDELEA KIMATAIFA


 NYOTA wa Simba, Luis Miquissone amesema kuwa jina lake kutajwa kwenye kikosi bora ni mwanzo wake yeye kuendelea kupambana kwa ajili ya timu ili kuweza kufikia malengo ambayo yamepangwa.

Kiungo huyo mshambuliaji jina lake limetajwa mara mbili kwenye kikosi bora cha wiki kwenye mashindano yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika.

Mara ya kwanza alitajwa yeye pamoja na beki Joash Onyango na mara ya pili alitajwa yeye pamoja na beki Mohamed Hussein.

Luis kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi ametupia mabao mawili ilikuwa mbele ya Al Ahly pamoja na Al Merrikh na yote ilikuwa Uwanja wa Mkapa.

Kiungo huyo amesema:”Ni furaha kwangu kuwe kwenye kikosi bora na namna ambavyo ninatajwa inaongeza nguvu kwangu kufanya zaidi ya hapa na ninashukuru kwa sapoti ambayo ninapata, kazi inaendelea,”.

SOMA NA HII  SIMBA SC WATUMIA BILIONI 1 KUPATA USHINDI MECHI ZA CAF