Home Burudani BUSHOKE: MAGUFULI ALIKUWA MTETEZI WA WANYONGE

BUSHOKE: MAGUFULI ALIKUWA MTETEZI WA WANYONGE


 RUTHA Bushoke, msanii wa muziki wa kizazi kipya amesema kuwa Rais John Magufuli alikuwa ni mtetezi wa wanyonge hivyo kifo chake kimewaachia ganzi watu wengi.

Akizungumza na Saleh Jembe, Bushoke amesema kuwa kwa matendo ambayo alikuwa anayafanya enzi za uhai wake aliwapa nafasi kubwa wanyonge kuishi kwa tabasamu hivyo kuondoka kwake kumeacha ganzi ndani ya mioyo ya wengi.

“Ni wengi ambao alikuwa anawatetea na hakuna ambaye alikuwa haoni kazi yake aliyokuwa anafanya. Ukweli ni kwamba alikuwa ni mtetezi wa wanyonge na alikuwa anapenda kuona haki inatendeka.

“Pigo ambalo lipo kwenye mioyo ya wengi ni kubwa kwa kweli hakuna anayeweza kuficha hali hiyo, ameondoka wakati bado dunia ikiwa inamuhitaji,” amesema.

Bushoke ni miongoni mwa wasanii ambao wameandika wimbo maalumu kwa ajili ya kumenzi Magufuli ambaye leo Machi 24 mwili wake upo Mwanza kwa ajili ya wakazi wa hapo kutoa heshima za mwisho.

SOMA NA HII  RUSHA KETE NA UJIPATIE MSHIKO WA KUTOSHA KUTOKA KASINO YA MTANDAONI YA MERIDIANBET....