Home Uncategorized MBADALA WA KINDOKI HUYU HAPA, ASAINI MIAKA MIWILI JANGWANI

MBADALA WA KINDOKI HUYU HAPA, ASAINI MIAKA MIWILI JANGWANI

IMEELEZWA kuwa mlinda mlango wa Mbao FC, Metacha Mnata amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia klabu ya Yanga.

Yanga kwa sasa ipo kwenye mpango wa kusuka kikosi kipya kwa ajili ya msimu ujao ambapo kwenye sekta ya mlinda mlango walikuwa na tatizo baada ya Beno Kakolanya kuvunja mkataba hivyo Klaus Kindoki alikuwa bado ana makosa mengi ya kiufundi.

Metacha ambaye alikuwa Mbao kwa Mkopo akitokea Azam FC, mkataba wake tayari umeisha na kikosi chake cha Azam.


Mwenyekiti wa Mbao Solly Njash amesema kuwamkataba wao na Mnata ulikuwa ni wa mkopo hivyo bado alikuwa ni mali ya Azam FC na kama anakwenda Yanga itakuwa ni mipango yake mwenyewe.

“Mnata alikuwa nasi ametimiza majukumu yake vizuri hivyo mkataba wake nasi umekwisha kama amekwenda kujiunga na Yanga ni maamuzi yake pamoja na timu yake ya zamani, sisi tunamtakia kila la kheri,” amesema.

SOMA NA HII  SIMBA YATOA TAMKO KUHUSU KUMSAJILI BERNARD MORRISON