Home Simba SC LUIS MIQUISSONE ANAONDOKA SIMBA, DAU LAKE NI NOMA

LUIS MIQUISSONE ANAONDOKA SIMBA, DAU LAKE NI NOMA


KUNA uwezekano mdogo sana kwa Klabu ya Simba kubaki na huduma ya nyota wao Luis Miquissone kwa msimu ujao ndani ya Ligi Kuu Bara kutokana na timu nyingi kuhitaji saini yake.

Miongoni mwa timu ambazo zinapewa nafasi kubwa ya kusepa na saini ya kiungo huyo ambaye wengi hupenda kumuita Konde Boy ni pamoja na Klabu ya Al Ahly.

Hivyo nyota huyo anaweza kuondoka ndani ya Simba ikiwa dau la timu ambazo zinamtazama zitakubalika ndani ya Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes.

Al Ahly ambayo ni klbu bora Afrika inatambua balaa la nyota huyo kwa kuwa aliwatungua Uwanja wa Mkapa dakika ya 30 akiwa nje ya 18 na kuwafanya waache pointi tatu jumla kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika, hatua ya makundi.

Bao lake hilo limetambuliwa na kuchaguliwa na Shirikisho la Soka Afrika,(Caf) kuwa bao bora la wiki huku jina lake pia likitajwa kwenye kikosi bora cha wiki pamoja na beki Joash Onyango ambaye naye yupo ndani ya Simba.

Mchezo wao ujao ni dhidi ya Al Merrikh ya Sudan ambao unatarajiwa kuchezwa Machi 6.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa sio Afrika pekee ambao wanamtazama Konde Boy bali hata nje ya nchi wapo mawakala wanaofuatilia kwa karibu mwendo wa nyota huyo.

“Sio Afrika pekee bali hata nje ya nchi hilo tunalijua na lipo wazi, lakini ili auzwe dau lake halitakuwa chini ya Euro milioni moja hivyo hilo ni la chini kabisakabisa,”

SOMA NA HII  KISA KUTOLEWA KLABU BINGWA...AHMED ALLY ASISITZA USAJILI MPYA SIMBA SC...ATAJA MASTAA...