Home epl MAGUIRE AGOMA KUOMBA MSAMAHA, ASEMA YEYE NI BEKI SIO MSHAMBULIAJI

MAGUIRE AGOMA KUOMBA MSAMAHA, ASEMA YEYE NI BEKI SIO MSHAMBULIAJI

 


HARRY Maguier, nahodha wa Manchester United amegoma kuomba msamaha kwa kushindwa kufunga bao kwenye mchezo wa Europa League hatua ya 16 bora dhidi ya AC Milan.

Beki huyo wa kati alikwama kubadili nafasi aliyopata kwa kupiga mpira uliogonga mwamba na kufanya United ilazimishe sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya AC Milan ndani ya Old Trafford. 

Ni Amad Diallo dakika ya 50 alifunga kwa United na Simon Kiaer dakika ya 90+2 kwa Milan aliweka usawa na kuipa kazi United kuwa na kibarua cha kusaka ushindi katika mchezo wa marudio unaotarajiwa kuchezwa Machi 18.

Maguire amesema: “Nilipaswa kufunga ila kwa hilo Siwezi kuomba msamaha kwa yoyote kwa ajili ya suala hilo.

“Ndio maana mimi ni beki sio mshambuliaji, lakini hakuna jambo la kuomba msamaha ilipaswa nifunge.

Maguire ameongeza kuwa United inahitaji kucheza vizuri kwa ajili ya mchezo wao ujao San Siro wiki ijayo ili kupata ushindi.


SOMA NA HII  MASHABIKI WACHOMA MOTO UWANJA...LIGI YA MABINGWA AFRIKA...ISHU NZIMA HII HAPA