Home Simba SC MASTAA SITA SIMBA WAIFUNIKA YANGA

MASTAA SITA SIMBA WAIFUNIKA YANGA

 


“WAMEFUNIKA” ndivyo unavyoweza kusema, kwani unaambiwa mastaa sita tu wa kikosi cha Simba wamefanikiwa kufunga mabao 36, ambayo ni idadi sawa na mabao yote yaliyofungwa na nyota wa kikosi cha klabu ya Yanga.

Mastaa hao sita wa Simba ni Meddie Kagere, John Bocco, Clatous Chama, Bernard Morrison, Chris Mugalu na Luis Miquissone.

Katika mchanganuo huo Kagere amefunga mabao 9 sawa na John Bocco, Clatous Chama 6, Chris Mugalu 5, Miquissone 4 na Morrison 3.

Simba ndiyo timu ambayo imefunga mabao mengi zaidi kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa na mabao 46 huku yanga wao wakiwa katika nafasi ya pili na mabao 36.

Simba pia ndiyo timu iliyofungwa mabao machache zaidi kwenye ligi, mabao 9 ikifuatiwa na Yanga waliofungwa mabao 14.

 

SOMA NA HII  MASHABIKI SIMBA WAMGEUKIA BOCCO...AONEKANA AKIWA NA KIKOSI B...KILA KITU HIKI HAPA