Home Yanga SC MWL KASHASHA : MICHAEL SARPONG BADO SANA, ANAKIMBIAKIMBIA UWANJANI TU

MWL KASHASHA : MICHAEL SARPONG BADO SANA, ANAKIMBIAKIMBIA UWANJANI TU

 


MCHAMBUZI wa masuala ya michezo Tanzania, Mwalimu Alex Kashasha amesema kuwa bado nyota wa Yanga, Michael Sarpong ana kazi ya kuonyesha uwezo wake kwa kuwa hakuna ambacho ameonyesha kwa sasa.


Sarpong raia wa Ghana, alisajiliwa na Yanga msimu huu akitokea Klabu ya Rayorn Sports ya Rwanda amekuwa kwenye wakati mgumu kwa kushindwa kufunga mabao ndani ya timu hiyo jambo ambalo linamkosesha furaha.

Chini ya Zlatko Krmpotic alitupia bao moja na zama za Cedric Kaze alitupia mabao matatu jambo ambalo linamfanya awe ametupia mabao manne na ana pasi moja ya bao.

Kuhusu uwezo wake Kashasha amesema:-“Huyu Michael Sarpong anapaswa kuonyesha uwezo wake ndani ya uwanja kwa kuwa bado kile ambacho mashabiki walitarajia angeonyesha ameshindwa kukitoa kwa wakati.
  
“Amecheza zaidi ya mechi 21 ana mabao manne, hivyo inaonekana anakimbiakimbia ndani ya uwanja nilazima Yanga wawe makini katika Scouting, hii itawafanya wawe wanapata wachezaji makini.
“Yanga ni timu kubwa na wachezaji wanaotakiwa kusajiliwa pale wanapaswa kuwa na hadhi kubwa ili watimize malengo ya timu kiujumla,” .
SOMA NA HII  WACHEZAJI HAWA WALIOACHWA NA SIMBA, YANGA WAPATA MAJANGA KATIKA USAJILI