Home Namungo FC NAMUNGO WATOA KAULI YA KIBABE WAKIJIANDAA DHIDI YA NKANA

NAMUNGO WATOA KAULI YA KIBABE WAKIJIANDAA DHIDI YA NKANA


KOCHA mkuu wa klabu ya soka ya Namungo, Hemmed Suleiman ‘Morocco’ ametamba kuwa, anaamini katika michezo yao minne ijayo ya hatua ya makundi kombe la Shirikisho Afrika vijana wake watafanya vizuri na kuwashangaza watu.

Namungo imeanza vibaya kwenye michezo yake ya hatua ya makundi ambapo wamepoteza michezo yote miwili ya kwanza, dhidi ya Raja Casablanca 1-0, na kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Pyramids.

Namungo ipo katika nafasi ya tatu ya kundi D la michuano hiyo wakiwa hawana pointi yoyote sawa na klabu ya Nkana kutokea Zambia, ambapo timu hizo zitavaana Aprili 2, mwaka huu katika uwanja wa Mkapa Dar es Salaam.

Akizungumzia mipango yao, Morocco amesema: “Tunaendelea na mazoezi ya kurekebisha pale ambapo tumeteleza, na kujiweka vizuri kwa ajili ya mchezo wetu ujao dhidi ya Nkana ambao tutacheza mwanzoni mwa mwezi Aprili.

“Kwetu tunaamini licha ya kwamba hatuko katika nafasi nzuri kwenye msimamo, lakini kuna matarajio makubwa ya kuweza kufanya vizuri katika michezo yetu minne iliyosalia na kupata matokeo ya kuwashangaza watu ambao wanadhani hatuna nafasi ya kusonga mbele.

SOMA NA HII  WAKATI YANGA WAKIALIKWA MALAWI...BURUNDI WAIPA SHAVU NAMUNGO...