Home Simba SC SVEN AIPELEKA SIMBA SC FIFA

SVEN AIPELEKA SIMBA SC FIFA


UNAAMBIWA aliyekuwa kocha wa Simba SC, Sven Vandenbroeck anayefundisha kwa sasa FAR Rabat iliyopo Ligi Kuu Morocco, amepeleka malalamiko yake FIFA ya kudai haki yake Msimbazi, ikiwamo posho.

Za chinichini imepenyezewa kwamba Sven anaidai Simba mkwanja wa maana, ingawa hakuna kigogo yeyote wa Msimbazi aliyethibitisha madai hayo.

Inasemekana Mbelgiji huyo alitaka kumalizana kwa amani na viongozi hao lakini kupigwa kwake kalenda juu ya malipo ya stahiki zake ndio kitu kilichomsukuma kukimbilia Fifa kudai chake.

Sven alitimka Simba mara baada ya kuisaidia timu hiyo kutinga hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa huku akieleza ameamua kuondoka nchini kutokana na matatizo ya kifamilia, japo siku chache aliibukia FAR Rabat.

SOMA NA HII  GOMES AWAWASHIA TAA YA KIJANI NDEMLA NA GADIEL MICHAEL