Home Yanga SC YANGA: MAGUFULI ALIKUWA NA BAHATI NA SISI

YANGA: MAGUFULI ALIKUWA NA BAHATI NA SISI

 

UONGOZI wa klabu ya soka ya Yanga, umesema kuwa miongoni mwa mambo ambayo wataendelea kuyakumbuka kuhusiana na Hayati Rais Dk. John Pombe Magufuli ni namna walivyokuwa na bahati naye.

Rais Magufuli alikuwa sehenu ya mashuhuda wa mchezo wa dabi ya Kariakoo iliyopigwa Machi 8, mwaka jana na kuwakutanisha wababe wa viunga vya Kariakoo klabu za Simba na Yanga ambapo Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Akitoa salamu za rambirambi kwa niaba wa uongozi wa Yanga, Kaimu Katibu Mkuu wa Yanga, Haji Mfikirwa amesema: “Sisi kama klabu ya Yanga kwa umoja wetu, tumepokea kwa masikitiko kifo cha Rais Magufuli kwa kuwa alikuwa sehemu ya faraja yetu. 

“Tunatoa salamu za pole kwa Serikali ya Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu, wanafamilia na Watanzania wote kwa ujumla kufuatia msiba huu, nasi tutaendelea kumkumbuka sana kwani mara zote alipokuja uwanjani tulikuwa na matokeo bora ikiwemo dhidi ya mtani wetu Simba.”

SOMA NA HII  WAKATI MASTAA SIMBA WAKITAMBA...MAYELE KAWASIKILIZA WEE....KISHA 'SIMPO' TU KAWAJIBU HIVI...