Home Yanga SC YANGA: TUNAAMINI YALIYOFANYWA NA MAGUFULI YATAENDELEA KUTENDEKA ILI KUMUENZI

YANGA: TUNAAMINI YALIYOFANYWA NA MAGUFULI YATAENDELEA KUTENDEKA ILI KUMUENZI


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa unaamini yale ambayo yalikuwa yanafanywa na Rais John Pombe Magufuli ambaye ametangulia mbele za haki yataendelea kufanyika kila wakati ili kumuenzi shujaa wa Afrika.

Magufuli alitangulia mbele za haki Machi 17 kwa maradhi ya moyo na Serikali imetangaza siku 21 za maombolezo ambapo leo Machi 22, mwili wake upo makao makuu ya Tanzania, Dodoma.

Jana Machi 21 ilikuwa ni zamu ya wakazi wa Dar kutoa heshima za mwisho ambapo maelfu ya watu walijitokeza kutoa heshima za mwisho, Uwanja wa Uhuru.

Miongoni mwa wale ambao walijitokeza pia ilikuwa ni pamoja na uongozi, wachezaji pamoja na mashabiki wa Yanga ambao walipata muda wa kutoa heshima za mwisho kisha kuelekea ofisi ya Chama Cha Mapinduzi, (CCM) kusaini kitabu cha maombolezo.

Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema:”Tumempoteza shujaa ambaye alikuwa ni kiongozi mpenda maendeleo na watu alikuwa anawepande pia kwa kuwa ameondoka basi hakuna namna nyingine zaidi ya kumuombea.

“Pia tuna amini kwamba yale ambayo alikuwa akiyafanya yataendelea kutimizwa kwa vitendo kwa kuwa Serikali bado ipo na watendaji wake ambao alikuwa akifanya nao kazi bado wapo,” .

SOMA NA HII  KWISHA KAZI....VIGOGO WAZITO YANGA SC WAITIBULIA AZAM FC KWA FEI TOTO...