Home CAF CAF WAJA NA SHERIA MPYA BAADA YA SIMBA KUTINGA ROBO FAINAL CAF

CAF WAJA NA SHERIA MPYA BAADA YA SIMBA KUTINGA ROBO FAINAL CAF


Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limepanga kuja na muongozo mpya wa usimamiaji wa vipimo vya ugonjwa wa Covid-19 kutokana na changamoto bnyingi zilizoibuka katikia mashindano yake mbalimbali inayoyasimamia.;

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya CAF, Alexander Siewe imesema kuwa shirikisho hilo linaandaa utaratibu mpya wa vipimo vya Covid-19 siku za usoni ili kuepusha migongano na malalamiko mengi kama ilivyotokea katika mashindano yake tofauti msimu huu.

“Kwa changamoto zilizoibuliwa kuhusiana na Covid-19 na vipimo vya PCR vinavyohitajika kwenye mashindano, mjadala umefikia makubaliano ya kutengeneza ushirikiano kwa kushirikiana na WHO (Shirika la Afya Duniani) na vyombo huru katika ufanyaji vipimo kabla ya mechi na hii itahusisha pia Fainali za Mataifa ya Afrika (Afcon) Cameroon,” imesema taarifa hiyo.

Hivi karibuni kumekuwa na malalamiko mengi ya timu mbalimbali za taifa na klabu juu ya vipimo vya Covid-19 zikidai vimekuwa vikitumika na timu wenyeji katika kuzidhohofisha timu pinzani katika mashindano mbalimbali yaliyo chini ya shirikisho hilo.

Machi 30, mchezo wa kuwania kufuzu Afcon baina ya wenyeji Sierra Leone na Benin wa kundi L ulishindwa kufanyika baada ya wageni kulalamikia majibu ya vipimo vya Covid-19 yalioonyesha wachezaji sita wao sita wana maambukizi ya virusi vya ugonjwa huo huku wenyewe wakidai wachezaji hao walikuwa wazima.

Siku moja kabla ya mechi hiyo, kiungo wa Uganda, Lwanga Taddeo nusura aikose mechi ya timu yake ugenini dhidi ya Malawi baada ya vipimo kuonyesha kuwa ameambukizwa Covid-19 lakini alipopimwa kwingine alionekana hajaambukizwa ugonjwa huo.

Kabla ya hapo, wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Simba walituhumiwa na Al Merrikh ya Sudan kuwa iliwahujumu katika majibu ya vipimo vya Covid-19 yaliyoonyesha wachezjai wake tisa wana maambukizo na hivyo kuwafanya wakose mechi baina ya timu hizo iliyochezwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Machi 16 ambao Simba iliibuka na ushindi wa mabao 3-0. 

Hata hivyo CAF ilitupilia mbali malalamiko hayo ya Al merrikh na kuisafisha Simba juu ya tuhuma hizo.

SOMA NA HII  LICHA YA SIMBA KUTINGA HATUA YA MAKUNDI ROBERTINHO AWAJIA JUU WACHEZAJI