KIUNGO mshambuliaji wa Azam FC, Idd Seleman, ‘Nado’ amesema kuwa sababu kubwa iliyomfanya aweze kuongeza mkataba wa kuendelea kukitumikia kikosi hicho ni makubaliano waliyofikia na uongozi na kuahidi kuzidi kupambana.
Jana, Aprili 13, Nado alisaini dili jipya la miaka miwili kwa kuboresha mkataba wake ambao ulikuwa unakaribia kufika ukingoni.
Nado alisaini mkataba huo mbele ya Ofisa Mtendaji Mkuu, Abdulkarim Amin ‘Popat’, utakaomfanya aendelee kusalia Azam FC hadi mwaka 2024.
Kiungo huyo ambaye aliibuka ndani ya Azam FC akitokea Klabu ya Mbeya City amehusika kwenye mabao 12, ametupia mabao 7 na pasi tano za mwisho kati ya mabao 36.
Nado amesema:”Bado niponipo kwa sasa Azam na ninapenda kuwaambia kwamba mashabiki nimeongeza mkataba wangu kwa miaka miwili baada ya kuzungumza kwa kina na viongozi, hivyo nina miaka mitatu hapa Azam.
“Awali mkataba wangu ulikuwa umebaki na mwaka mmoja, nipo Azam na ninafurahi kuwa hapa nina amini kwamba nitaendelea kupambana kwa sababu mimi ni mpambanaji,” .