Home Simba SC GOMES WA SIMBA AWACHAMBUA WAPINZANI WAO KIMATAIFA

GOMES WA SIMBA AWACHAMBUA WAPINZANI WAO KIMATAIFA

 


KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa amewaambia wachezaji wake wanapaswa kuonyesha ukubwa walionao kwa kupata matokeo chanya kwenye mechi zote za ligi pamoja na zile za kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tayari Simba imetinga hatua ya robo fainali ikiwa inaongoza kundi A na pointi 13 inafuatiwa na vigogo Al Ahly ambao wana pointi 11 wakiwa nafasi ya pili. Aprili 30 inatarajiwa kuchezwa droo ya michuano hiyo mikubwa.

Gomes amesema kuwa anasubiri kuona wapinzani atakaopangiwa kucheza nao huku akibainisha kuwa wote anawatambua kutokana na kuwa na data zao pamoja na uzoefu wa soka la Afrika.

“Ukizungumza kuhusu Simba kwa sasa ni moja ya timu kubwa Afrika, hivyo nimewaambia wachezaji kwamba lazima waonyeshe ukubwa wao kwenye mechi zote ambazo tutacheza iwe ni kwenye ligi ama robo fainali.

“Kwa wakati huu tunawekeza nguvu zetu kwenye mechi za ligi ila haina maana kwamba tutapuuzia kuhusu mechi zetu za robo fainali kwani hiyo nayo ni mipango yetu kuona kwamba tunafanya vizuri.

“Natambua soka la Afrika vizuri na changamoto zake, nimefundisha Algeria ninazitambua timu za huko namna ilivyo na Afrika Kusini pia nina marafiki na data zao ninazo hivyo hakuna haja ya kuwa na hofu katika hilo,” amesema.  

Timu ambazo zinaweza kukutana na Simba kwenye hatua ya robo fainali ni pamoja na CR Belouizdad ipo nafasi ya 10 na pointi 26 baada ya kucheza mechi 15 na MC Alger ipo nafasi ya 11 na pointi 25 baada ya kucheza mechi 16 hizi ni za Algeria na Kaizer Chiefs ni ya Afrika Kusini ipo nafasi ya 9 na pointi 24 baada ya kucheza mechi 20.

Gomes ameweka wazi kuwa aliwahi kufundisha soka nchini Algeria hivyo hana mashaka ikiwa atakutana na timu za kutoka huko kwenye hatua ya robo fainali na kwa Kazier Chiefs hana tatizo nao.

Timu ambayo aliwahi kuifundisha Gomes nchini Algeria inaitwa CS Constantine ilikuwa ni msimu wa 2015/16 ambayo kwa sasa ipo nafasi ya 8 na pointi zake 30 baada ya kucheza mechi 19.

SOMA NA HII  KOCHA SIMBA ATAJA SIFA ZA WACHEZAJI ATAKAOWATUMIA