Namungo FC

SERIKALI YAITAKA YANGA, NAMUNGO KUIGA MFANO WA SIMBA

admin April 21, 2021 9:48 pm

 Waziri wa Maliasili na Utalii, Dkt.Damas Ndumbaro amezitaka timu za  Yanga  na Namungo kuiga mfano wa timu ya Simba katika kutangaza utalii wa Tanzania kupitia jezi zao ambazo zimeandikwa Visit Tanzania. 


Ndumbaro amesema  kuwa  wao hawachagui timu yoyote ya kufanya nayo kazi ,kwahiyo waliopo tayari wakaribie ofisini kwetu ili waweze kuitangaza Tanzania kitaifa na kimataifa. 


Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania katika Ligi ya Mabingwa Afrika wapo hatua ya robo fainali katika ligi hiyo yenye ushindani ambapo ilikuwa inavaa jezi zenye neno Visit Tanzania.


Ndumbaro amesema:”Simba ndiyo walikuja  kuomba nafasi hiyo na wala hatujawapa pesa wanatangaza bure hivyo timu zingine zisiogope kuja hii ni fursa ya kutangaza utalii wa nchi yetu, ” amesema Ndumbaro.


Namungo inapeperusha bendera katika Kombe la Shirikisho ikiwa ipo hatua ya makundi, Yanga kwa sasa inapambana kutwaa taji la ligi ili iweze kurejea katika mashindano ya kimataifa.

UONGOZI WA YANGA KUKETI NA NTIBANZOKIZA ILI KUJUA TATIZO LIPO WAPI MAMBO YANAZIDI KUPAMBA MOTO, CHEKI MSIMAMO ULIVYO BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply