KOCHA Msaidizi wa Simba SC, Seleman Matola amesema kuwa wapinzani wao kwenye ligi, wasitarajie kuona Simba SC ikishuka kwenye nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi.
Baada ya mechi ya jana dhidi ya Dodoma Jiji, Simba SC imezidi kujiimarisha kwenye msimamo wa ligi, ikiwa na alama 61, wakati wapinzani wao wa karibu ni Yanga wenye alama 57.
Matola amesema,kwamba kwa sasa mipango yao ni kushinda mechi hizo ikiwemo zile za viporo kwa ajili ya kuendelea kukaa kileleni.
βMipango yetu kwa sasa ni kukaa kileleni na hatutashuka hadi tunachukua ubingwa wakati msimu ukiisha.
Sisi tungekaa kwenye nafasi hii muda mrefu lakini mechi zetu za kimataifa zilikuwa zinatuchelewesha na kusababisha tuwe na viporo.
βKwa sasa tutapambana tusitoke tena hadi mwisho wa msimu katika nafasi ambayo tupo na tutahakikisha mechi zetu zote ambazo ziko mbele tunashinda,β alimaliza