Home Ligi Kuu DIDA: TUNAHITAJI KUBAKI NDANI YA LIGI KUU BARA, TUTAPAMBANA

DIDA: TUNAHITAJI KUBAKI NDANI YA LIGI KUU BARA, TUTAPAMBANA


 DEOGRATIUS Munish,’Dida’ kipa namba moja wa Klabu ya Ihefu amesema bado timu hiyo ina nafasi ya kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2021/22.

Kwa sasa Ihefu FC inapambana kusaka nafasi ya kubaki ndani ya ligi kwa kuwa imekuwa na mwendo wa kusuasua.

Imekusanya pointi 20 ipo nafasi ya 17 baada ya kucheza jumla ya mechi 24. 

Dida amesema:”Tupo kwenye mapambano kwa sasa na ninaona kwamba wachezaji wanahitaji kubaki ndani ya ligi hili ni lengo la kila mmoja na inawezekana.

“Ninaamini kwamba tukijitahidi kwa juhudi kwenye mechi zetu na kupata matokeo mazuri tutabaki kwenye ligi na kila mmoja anapenda kuona hilo linatokea,” .

Mchezo wake ujao kwenye ligi itakuwa ugenini dhidi ya Namungo FC na unatarajiwa kuchezwa Aprili 8, Uwanja wa Majaliwa.

SOMA NA HII  LIGI KUU BARA: YANGA 3-3 KAGERA SUGAR