Home Ligi Kuu HITIMANA ATUMIWA TIKETI KUIMALIZA SIMBA

HITIMANA ATUMIWA TIKETI KUIMALIZA SIMBA

 


BAADA ya kutoka taarifa kuwa kocha wa Mtibwa Sugar Hitimana Thiery amegoma kurejea kwenye timu hiyo, uongozi wa timu hiyo umesema kuwa umefanya mchakato wa kumtumia kocha huyo tiketi ili aiwahi Simba.

Hayo yamesemwa na msemaji wa timu hiyo Thobias Kifaru ambaye aliweka bayana taarifa za kocha huyo kushindwa kurejea kwenye timu ni kweli, lakini viongozi wapo kwenye jitihada za kumaliza tofauti iliyotokea ili aweze kurejea kwenye timu.

Akizungumzia ishu hiyo Kifaru amesema: “Ni kweli kumekuwepo taarifa za kocha wetu Hitimana Thiery kukataa kurejea nchini kutokea kwao Rwanda alikokwenda kwa ajili ya mapumziko ya siku 21 za maombolezo ya Hayati Dk John Pombe Magufuli, lakini nikuambie uongozi wa Mtibwa upo kwenye harakati za kutuma tiketi ya ndege ili kocha huyo arejee nchini.

“Tunataka aje kukinoa kikosi kwani April 14 tutakuwa na mchezo muhimu dhidi ya Simba, kwahiyo lazima yeye awepo kwenye benchi la ufundi la timu yetu,” amesema Kifaru.

Alipotafutwa Hitimana mwenyewe, simu yake iliita bila kupokelewa. Inatajwa kuwa Hitimana amegoma kurejea nchini kutokana na kile kinachodaiwa kuchoshwa na kuingiliwa majukumu yake ya ukocha na viongozi wa timu hiyo.

SOMA NA HII  KISA NEMBO YA MDHAMINI WA LIGI KUU NBC...BODI LA LIGI KUZISHUSA DARAJA TIMU ZA LIGI KUU