Home Yanga SC JOB AMPA TANO MWAMBUSI YANGA

JOB AMPA TANO MWAMBUSI YANGA


BEKI mpya wa klabu ya Yanga, Dickson Job amesifu mbinu zinazotumiwa na Kaimu kocha mkuu wa kikosi hicho, Juma Mwambusi na kusema kuwa ana imani kubwa kwa maandalizi wanayoyafanya watapata matokeo mazuri katika michezo yao ijayo.

Yanga imejichimbia katika mji wa Avic, Kigamboni jijini Dar es Salaam ambapo wanajifua vikali kwa ajili ya michezo yao ya Ligi Kuu Bara na kombe la Shirikisho maarufu kombe la FA, ambapo wanatarajia kuanza vibarua hivyo kwa kucheza dhidi ya KMC Jumamosi hii ya Aprili 10.

Tangu asajiliwe na Yanga akitokea ndani ya kikosi cha Mtibwa Sugar aliyoichezea kwa mafanikio tangu mwaka 2016, Job aliyerudi kutoka kwenye majeraha hajaichezea Yanga mchezo wowote kutokana na majeraha ya misuli ambayo yalimuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu tangu mwezi Januari mwaka huu.

Akizungumzia maandalizi yao Job amesema: “Tunaendelea vizuri na maandalizi ya michezo yetu ijayo ya Ligi Kuu pamoja na kombe la FA, tumekuwa na muda mrefu wa maandalizi chini ya kocha Mwambusi.

“Kocha amerekebisha vitu vingi tangu apewe kikosi katika maeneo mbalimbali ikiwemo kutuongezea hali ya kujiamini na mbinu za kusaka ushindi hivyo, naamini tutaonyesha mabadiliko makubwa kwenye michezo yetu ijayo,”

SOMA NA HII  BAADA YA YANGA KULA KICHAPO...SHABIKI HUYU MWANACHI AFARIKI...ISHU NZIMA IKO HIVI