Home epl MANE NA SALAH WAAMBIWA KWAMBA SIO WASHAMBULIAJI HALISI

MANE NA SALAH WAAMBIWA KWAMBA SIO WASHAMBULIAJI HALISI


 MICHAEL Owen amesema kuwa nyota wawili wa Liverpool, Mohamed Salah na Sadio Mane sio washambuliaji halisi katika utendaji wao wa kazi ilikuwa ni mara baada ya sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Newcastle.

Salah licha ya kutupia bao mapema dakika ya tatu alishindwa kuongeza bao la pili na mabeki wa Liverpool walizidiwa ujanja na kuruhusu bao la dakika za lala sama kuweka usawa.

Mabingwa hao watetezi walikwama wakiwa pale Uwanja wa  Anfield baada ya kuokota bao la Joe Willock dakika ya 90+5.

Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha Manchester United amesema kuwa alishtushwa na matokeo hayo ambayo walipata timu hiyo.

“Kuna tatizo ninaona hasa kwa Mane ambaye ni mchezaji mwenye uwezo ila alishindwa kufunga, Salah ni mchezaji mzuri inaamini kwa kuwa amefunga mabao mengi hilo ni jambo zuri.


“Lakini katika hayo hakuna ambaye ni mshambuliaji halisi, ni wachezaji ambao huwezi kuwaweka katika eneo hilo na kuamini kwamba wanaweza kufanya vizuri zaidi.


“Wameshindwa kuwa na mwendelezo mzuri wa kufunga mabao licha ya kwamba Liverpool imekuwa ikitengeneza nafasi nyingi,” amesema.

 


SOMA NA HII  LIVERPOOL YAPIGWA MARUFUKU KUKANYAGA UJERUMANI