Home kimataifa MBAPPE AITIKISA KIMTINDO PSG, KUTOCHEZA OLYMPIC

MBAPPE AITIKISA KIMTINDO PSG, KUTOCHEZA OLYMPIC


 MSHAMBULIAJI wa Klabu ya PSG, Kylian Mbappe raia wa Ufaransa ameliambia Shirikisho la Soka Ufaransa kwamba hatakuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Ufaransa kwenye michuano ya Olympic.

Michuano hiyo mikubwa inatarajiwa kufanyika Julai, mwaka huu 2021 Tokyo, Japan ambapo nyota huyo amesema kuwa anataka kutuliza akili ili kuamua hatma yake ndani ya PSG.

Mshambuliaji huyo amebakiza mwaka mmoja katika mkataba wake ndani ya kikosi hicho kinachoshiriki Ligue 1.

Nyota huyo anatajwa kuingia kwenye rada za Klabu ya Real Madrid inayoshiriki La Liga bado hajaamua hatma yake kuhusu maisha yake mapya wakati ujao.

“Ninatakiwa kufikiria nini kitakuwa mbele yangu kwa siku zijazo, hivyo nahitaji kutulia kuamua hatma yangu,” . 

SOMA NA HII  ATLETICO MADRID YATWAA UBINGWA, SUAREZ SHUJAA