Home Yanga SC YANGA YATEMBEZA KICHAPO, YASHINDA MABAO 3-0 DHIDI YA AFRICAN LYON

YANGA YATEMBEZA KICHAPO, YASHINDA MABAO 3-0 DHIDI YA AFRICAN LYON


KIKOSI cha Yanga kinachonolewa na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi kimezidi kujinoa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho kikiwa kimeweka kambi yake Kigamboni, kijiji cha Avic.

Jana Aprili 6 kilicheza mchezo wa kirafiki dhidi ya African Lyon ikiwa ni kujiweka sawa kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya KMC.

Kwenye mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 ambapo mabao ya Yanga yalifungwa na Michael Sarpong, Fiston Abdulzack pamoja na Paul Godfery, ‘Boxer’.

Yanga inakumbuka kwamba ilipokutana na KMC kwenye mchezo wao wa mzunguko wa kwanza Uwanja wa CCM Kirumba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 hivyo itaingia uwanjani kulinda rekodi huku KMC ikihitaji kutibua rekodi hiyo.

Mwambusi amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na morali ya wachezaji ni kubwa.

“Morali ya wachezaji ni kubwa na kila mmoja anaonekana kuwa na furaha hivyo tutapambana kupata matokeo,” .

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Aprili 10, Uwanja wa Mkapa majira ya saa 1:00 usiku. 


SOMA NA HII  NABI AWAFUNGIA KAZI WANIGERIA..DITRAM NCHIMBI 'DUMA' APEWA KAZI MAALUMU