Home Ligi Kuu IHEFU FC YAZITAKA POINTI TATU ZA NAMUNGO

IHEFU FC YAZITAKA POINTI TATU ZA NAMUNGO


 ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa Ihefu FC yenye maskani yake Mbeya amesema kuwa wanahitaji pointi tatu muhimu kwenye mchezo wao wa ligi dhidi ya Namungo FC utakaochezwa Uwanja wa Majaliwa.

Ihefu kwenye msimamo ipo nafasi ya 17 ina pointi 20, inakutana na Namungo FC iliyo nafasi ya 10 na pointi zao kibindoni ni 27.

Akizungumza kuelekea kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuchezwa Aprili 8, Katwila amesema kuwa wanachohitaji kwenye mchezo huo ni pointi tatu.

“Tupo kwenye nafasi mbaya kwa sasa tunapambana ili tujinasue hapa tulipo, hivyo nimewaambia wachezaji wanapaswa wajiamini na tupambane kupata pointi tatu kwenye mechi zetu.

“Haitakuwa kazi rahisi hasa ukizingatia kwamba mzunguko wa pili kila timu inahitaji pointi tatu. Mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kitakuwa sawa,”. 

Kwenye msimao wa ligi, Ihefu FC ipo nafasi ya 17 na pointi 20 inakutana na Namungo FC iliyo nafasi ya 10 na 27.

SOMA NA HII  BILIONI 225.6 ZA AZAM MEDIA ZILETE CHACHU YA MAFANIKIO KWENYE SOKA LETU